DC apania kuondoa aibu ya mauaji ya vikongwe

Muktasari:

Alisema kukatwa mapanga kwa vikongwe ni aibu  kwa Taifa, hivyo kila mmoja awe mlinzi  ili mzee asidhuriwe.

Shinyanga. Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amesema amedhamiria kuliondolea Taifa aibu ya mauaji ya vikongwe.

Alisema kukatwa mapanga kwa vikongwe ni aibu  kwa Taifa, hivyo kila mmoja awe mlinzi  ili mzee asidhuriwe.

Aliwataka viongozi, wanasiasa na jamii kulilinda kundi hilo  kwa nguvu zote.