DC apiga marufuku biashara ya mkaa nje ya Wilaya

Muktasari:

Ameoa tamko hilo alipotembelea miradi ya  ofisi ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS).

Manyoni. Mkuu wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida, Geofrey Mwambe amepiga marufuku usafirishaji mkaa nje  ya wilaya hiyo.

Ametoa tamko hilo alipotembelea miradi ya  ofisi ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS).

“Najua Tanzania haijafikia hatua ya kila wananchi kutumia nishati mbadala, hivyo ili kulinda uoto wa asili na misitu, mkaa uchomwe kwa matumizi ya nyumbani na kwa biashara ya ndani siyo kusafirisha nje ya wilaya,” amesema Mwambe.

Katika harakati za kupambana na biashara ya usafirishaji mkaa, TFS Wilaya ya Manyoni imekamata zaidi ya magunia 200 ya mkaa na mbao 70 zilizokuwa zikisafirishwa.