DC kujitosa kufundisha wanafunzi darasani

Muktasari:

  • Akifungua mafunzo kwa walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Nkulu amesema uamuzi wake unalenga kuhakikisha wanafunzi hawakosi masomo kwa sababu ya uhaba wa walimu.

Kahama. Kutokana na upungufu wa walimu wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga, Mkuu wa wilaya hiyo, Fadhili Nkulu ameahidi kuingia darasani kufundisha wanafunzi.

Akifungua mafunzo kwa walimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Nkulu amesema uamuzi wake unalenga kuhakikisha wanafunzi hawakosi masomo kwa sababu ya uhaba wa walimu.

“Kama kutatokea uhaba wa walimu katika wilaya yangu, nitajitolea kuingia darasani kufundisha kuliko wanafunzi kupitisha vipindi bila masomo,” amesema Nkulu.

Amesema walimu wanaohudhuria mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi kwa uratibu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tea) kuwa atafanya hivyo kwa sababu kitaaluma ni mwalimu.