DC mpya aahidi kurejesha hadhi ya Arusha

Muktasari:

  • Akizungumza baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo  alisema kwa kushirikiana na viongozi wengine wataweza kuwapa wananchi kile wanachokitegemea katika serikali ya wamu ya tano.

Arusha. Mkuu mpya wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro amesema moja ya majukumu atakayoyapa kipaumbele katika uongozi wake ni kuirejesha hadhi ya jiji la Arusha kuwa kama lilivyokua awali kwa kuimarisha hali ya usalama na utulivu.

Akizungumza baada ya kuapishwa na Mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo  alisema kwa kushirikiana na viongozi wengine wataweza kuwapa wananchi kile wanachokitegemea katika serikali ya wamu ya tano.

 "Napenda kumshukuru mheshimiwa Rais kwa kuniamini na kuniteua katika nafasi hii muhimu, napenda kumhakikishia nitatumia maarifa yangu ambayo nimeyapata kwa kipindi cha muongo mmoja nilichokua nikifanya kazi Ikulu kutoa utumishi uliotukuka na nitashirikiana na viongozi wote akiwemo Mstahiki Meya Kalist Lazaro kuwaletea wananchi maendeleo," alisema.

Hivi karibuni Rais John Magufuli alitengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda na kumteua aliyekua Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Mrisho Gambo.

Kwa habari zaidi nunua gazeti la Mwananchi kesho, kwa walio mbali wanaweza kujiunga na  epaper yetu kwakubonyeza hapa, Kwa kupata BreakingNews andika neno HABARI tuma kwenda 15569, Sh. 150/- kwa siku.