Daraja la Tuangoma kugharimu Sh 266 bilioni

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tamisemi  Selemani Jaffo akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa uboreshaji wa miji DMDP,Tuangoma,Wilaya ya Temeke.Picha na Herieth Makweta.

Muktasari:

  • Fedha hizo ni za miradi ya uboreshaji miji (DMDP) inayosimamiwa na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – Tamisemi.
  • Kiasi hicho ni wastani wa asilimia 45 ya fedha yote ya mradi kutoka Benki Kuu ya Dunia ambayo ilisaini mkataba wenye jumla ya Dola za Marekani 300 milioni, sawa na Sh600 bilioni kwa ajili ya kutekeleza mradi wa DMDP katika serikali za mitaa za mkoa wa Dar es Salaam.

Dar es Salaam. Daraja lenye urefu wa mita 800 linatarajiwa kujengwa katika Kata ya Tuangoma, Wilaya ya Temeke na litagharimu kiasi cha Sh266 bilioni.

Fedha hizo ni za miradi ya uboreshaji miji (DMDP) inayosimamiwa na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – Tamisemi.

Kiasi hicho ni wastani wa asilimia 45 ya fedha yote ya mradi kutoka Benki Kuu ya Dunia ambayo ilisaini mkataba wenye jumla ya Dola za Marekani 300 milioni, sawa na Sh600 bilioni kwa ajili ya kutekeleza mradi wa DMDP katika serikali za mitaa za mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza kwenye ukaguzi wa mradi huo ulioanza kutekelezwa katika Kata hiyo, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tamisemi Selemani Jaffo alitahadharisha umakini katika ujenzi huo kwa kuzingatia viwango.

Hata hivyo alitoa rai kwa wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu  inayojengwa na serikali, kwani walinzi wa miradi hiyo ni wananchi wenyewe.

“Kuna tatizo la uharibifu wa miundombinu inayojengwa na serikali, walinzi wa mradi huu ni wananchi wenyewe,” alisema na kuongeza;