Darasa la nne, saba ni ujiko

Muktasari:

  • Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo iliyoanzishwa miaka tisa iliyopita, Papias Anthony alisema ni darasa la saba na nne pekee, wanaotumia hayo madarasa yaliyojengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.

Muleba. Wanafunzi 430 kati ya 510 wa Shule ya Msingi Kabasharo, Kijiji cha Kyota, Tarafa ya Kimwani wilayani Muleba mkoani Kagera, wanasoma kwenye viwanja vya michezo kutokana na shule hiyo kuwa na madarasa mawili pekee.

Kaimu Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo iliyoanzishwa miaka tisa iliyopita, Papias Anthony alisema ni darasa la saba na nne pekee, wanaotumia hayo madarasa yaliyojengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Muleba.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kyota, Daudi Kiluma alisema tayari uongozi wa kijiji kwa kushirikiana na wananchi na wadau wengine, umefanikiwa kupata Sh4.8 milioni zitakazotumika kujenga madarasa.

Mkuu wa Wilaya ya Muleba, Henry Ruyango aliuagiza uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo kushughulikia changamoto zinazoikabili shule hiyo.