Dart yasaka mzabuni wa kadi za mabasi

Muktasari:

  • Rwakatare alisema kwamba lengo lao ni kupata kampuni ambayo itasimamia utengenezaji wa kadi hizo ili iweze kutolea majibu linapotokea tatizo lolote.

Mkurugenzi Mkuu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Ronald Rwakatare amesema mchakato wa kutafuta mzabuni wa kusimamia utengenezaji wa kadi bado unaendelea.

Rwakatare alisema kwamba lengo lao ni kupata kampuni ambayo itasimamia utengenezaji wa kadi hizo ili iweze kutolea majibu linapotokea tatizo lolote.

“Tunaomba radhi kwa ucheleweshaji wa upatikanaji wa kadi hizo kwa kuwa ni jambo nyeti linalohusisha suala la mambo ya fedha,” alisema.

Hadi kufikia Juni mradi huo ulikuwa unasafirisha watu 200,000 kwa siku kutoka watu 50,000 waliokuwa wakisafirisha mwaka jana mradi ulipoanza kazi.