Dawa za mabusha, matende zaanza kutolewa Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akimeza dawa za kingatiba za minyoo ya tumbo, matende na mabusha ambapo zitatolewa kwa siku tano katika maeneo tofauti jijini hapa. Picha na Muyonga Jumanne

Muktasari:

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Grace Maghembe kuwa mwaka 2015 lengo ilikuwa kugawa dawa kwa watu milioni 4 ila waligawa kwa watu milioni 3.9 sawa na asilimia 80.

Dar es Salaam. Wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam wametakiwa kujitokeza kumeza dawa za kinga ya mabusha na matende ili kujikinga na magonjwa hayo katika vituo 957 vya kudumu vilivyoweka.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Grace Maghembe kuwa mwaka 2015 lengo ilikuwa kugawa dawa kwa watu milioni 4 ila waligawa kwa watu milioni 3.9 sawa na asilimia 80.

"Mwaka huu lengo letu ni kugawa kwa watu milioni 4 ila muitikio wa wamama umekuwa mdogo niwaambie kuwa mabusha yanawapata hata wao kwenye sehemu za siri na maziwa," alisema Magembe.

Katika kuboresha zoezi hilo tayari wameanzisha vituo viwili kwa ajili ya kufanya upasuaji wa mabusba ambavyo viko Pugu na Mbweni na watu 104 washafanyiwa upasuaji.

Habari Zinazohusiana