VIDEO: Kiatu cha Diamond chakatika mahakamani

TAZAMA KILICHOMTOKEA DIAMOND HADI KUVUA MAKOBAZI ALIPOWASILI MAHAKAMANI LEO

Muktasari:

Alikuwa anahudhuria kesi dhidi yake iliyofunguliwa na Hamisa Mobeto kuhusu matunzo ya mtoto wake


Dar es Salaam. Msanii Diamond Platnumz leo Februari 8, 2018 amekumbana na masaibu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alikokwenda kusikiliza kesi inayomkabili ya matunzo ya mtoto Prince Abdul, baada ya  kiatu chake  kimoja cha wazi kukatika.

Baada ya tukio hilo, msanii huyo alilazimika kukaa katika moja ya mabenchi yaliyopo katika mahakama hiyo, alisaidiwa na mmoja wa watu alioongozana nao kukiweka sawa kiatu hicho.

Ufundi huo wa aina aina uliofanywa na msaidizi huyo wa Diamond, ulichukua takriban dakika tano kisha kumkabidhi msanii huyo kiatu hicho ambacho alikivaa na kuingia ndani ya chumba cha mahakama.

Diamond, yupo mahakamani hapo upande wa watoto kusikiliza kesi inayomkabili ya matunzo ya mtoto Prnce Abdul iliyofungulizwa na mwanamitindo Hamisa Mobeto.