Diamond kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa mume wa Zari

Muktasari:

Zari alizaa na Ivan watoto watatu kabla ya kukutana na Diamond ambaye amezaa naye watoto wawili.

Dar es Salaam. Staa wa muziki  Diamond Platnumz amethibitisha kuhudhuria mazishi ya Ivan Ssemwanga aliyekuwa mzazi mwenza Zari.

Zari alizaa na Ivan watoto watatu kabla ya kukutana na Diamond ambaye amezaa naye watoto wawili.

Diamond anahudhuria mazishi hayo kumpa pole na kuungana na mzazi mwenzake huyo waliyepata nae watoto wawili Tiffa na Nillan.

Diamond athibitisha kuwa atahudhuria katika mazishi mbele ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Nairobi katika kipindi cha The Trend kilichokuwa kinarushwa moja kwa moja kupitia kituo cha matangazo cha NTV cha nchini humo.

“Nilikuwa nimeingia mkataba wa kazi siku nyingi msiba umetokea ghafla hivyo siwezi kuahirisha shoo ya watu ninaweza kuonekana kwa mtizamo tofauti.

“Lakini niliongea na mzazi mwenzangu akanielewa lakini nikimaliza hapa shoo ya The Koroga Festival nitaenda Uganda kwa ajili ya mazishi na baada ya hapo ndio nitarudi nyumbani,” alisema Diamond.

Mjomba wa marehemu, Herbert Luyinda ameviambia vyombo vya habari nchini Uganda kuwa ibada takatifu ya kumuaga mpendwa wao itafanyika leo, kabla ya mazishi yatakayofanyika kesho  kijijini kwao Nakaliro.

Mitandao ya Uganda inadai Ivan alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya Shambulio la Moyo (Coronary Artery Disease).