Diddy asadia ujenzi wa wodi wa wanawake Uganda

Muktasari:

Diddy amesema anatoa kiasi hicho cha fedha kumuunga mkono rafiki yake na pia kuwahamasisha vijana wengine kushiriki katika kutatua matatizo yao wenyewe.

Rapa wa Mareakani, P Diddy ametoa mchango wa dola za Marekani 200,000 kusaidia ujenzi wa wodi ya wanawake nchini Uganda ikiwa ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na rafiki yake French Montana.

Diddy amesema anatoa kiasi hicho cha fedha kumuunga mkono rafiki yake na pia kuwahamasisha vijana wengine kushiriki katika kutatua matatizo yao wenyewe.

Mwaka jana rapa Fench Montana kupitia kampeni yake ya Unforgettable Healthcare akishirikiana na taasisi ya Mama Hope wamekuwa wakishiriki ujenzi wa wodi za wanawake nchini humo.

Mbali na Diddy, The Weekend alichangia dola 100,000 kuunga mkono jitihada hizo.