Diwani, mtendaji kortini kwa ubadhirifu

Muktasari:

Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Augustine Rwizile.

Arusha. Diwani wa Kata ya Daraja Mbili (Chadema), Prosper Msofe na Ofisa Mtendaji mstaafu wa kata hiyo, Modestus Lupogo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa tuhuma za ubadhirifu wa  Sh8 milioni za umma.

Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Augustine Rwizile.

Wakisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo, waendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Rehema Mteta na  Monica Kijazi walisema kosa la kwanza linamkabili Msofe kwa kutumia nyaraka kumdanganya mwajiri  kinyume na kifungu cha 22 cha Sheria ya Takukuru nambari 11 ya mwaka 2007. Kesi hiyo itatajwa Oktoba 21.