Dk Likwilile atumbuliwa Wizara ya Fedha na Mipango

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dk Servacius Likwelile

Muktasari:

  • Kabla ya uteuzi huo Doto alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera)..

Dar es Salaam. Rais Dk John Magufuli leo amemteua Doto James kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na ‘kumtema’ Dk Servacius Likwelile ambaye atapangiwa kazi nyingine..

Kabla ya uteuzi huo Doto alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango (Sera).

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU, Gerson Msigwa

Imeeleza kuwa  Doto ataapishwa kesho saa 2:45 Asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.