Dk Mpango aeleza Rais Magufuli aliyothubutu kufanya

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango akionyesha begi lililobeba hotuba ya Bajeti Kuu ya Serikali baada ya kuwasili kwa ajili ya kuiwasilisha Bungeni, jijini Dodoma leo. Picha na Edwin Mjwahuzi

Muktasari:

Rais ameweza kugharimia elimu msingi bure ambapo kila mwezi anatoa Sh20.8 bilioni.

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango ameeleza mambo 10 ambayo Rais John Magufuli amethubutu kuyafanya ikiwemo suala la kuhamisha makao makuu ya nchi kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma.

Mpango amesema hayo wakati akiendelea kusoma bajeti ya mwaka wa fedha 2018/19 leo Juni 14.

Mbali na kuhamishia makao makuu Dodoma pia ameeleza kuwa Rais Magufuli ameweza kujenga ukuta katika mgodi wa Mirerani uliogharimu Sh5.42 bilioni ili kudhibiti upotevu wa madini.

“Tangu ukuta huo umejengwa mapato ya madini yameongezeka kuliko mapato ya miaka mitatu.”

Pia amesema Rais ameweza kugharimia elimu msingi bure ambapo kila mwezi anatoa Sh20.8 bilioni.

“Kutokana na gharama hizo uandikishaji wa wanafunzi umeongezeka kutoka 448,600 hadi 672,692.”

Endelea kufuatilia habari zaidi zinakujia