Dk Possi ajiuzulu ubunge

Dk Abdallah Possi

Muktasari:

  • Uamuzi huo wa Dk Possi umekuja siku tatu baada ya Rais John Magufuli kumteua kuwa balozi.
  • Spika wa Bunge, Job Ndugai alithibitisha kupokea barua ya kujiuzulu ya mbunge huyo jana na kueleza kuwa nafasi yake imebaki wazi.

Dar es Salaam. Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu aliyekuwa akishughulikia Walemavu, Dk Abdallah Possi amemuandikia Spika wa Bunge barua ya kujiuzulu.

Uamuzi huo wa Dk Possi umekuja siku tatu baada ya Rais John Magufuli kumteua kuwa balozi.

Spika wa Bunge, Job Ndugai alithibitisha kupokea barua ya kujiuzulu ya mbunge huyo jana na kueleza kuwa nafasi yake imebaki wazi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Bunge, Spika Ndugai tayari amemuandikia barua Rais kumfahamisha juu ya kujiuzulu kwa Dk Possi kama mbunge wa kuteuliwa