Dk Shein amuapisha mwenyekiti ZEC

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein

Muktasari:

Pia amewaapisha wajumbe sita wa ZEC

Zanzibar. Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein leo Ijumaa Juni 22, 2018 amemuapisha Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid kuwa mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

 

Dk Shein pia amewaapisha wajumbe wa ZEC ambao kama ilivyo kwa Jaji mstaafu Hamid, nao aliwateua siku moja.

 

Wajumbe walioapishwa ni Mabruki Jabu Makame, Feteh Saad Mgeni, Makame Juma Pandu, Dk Kombo Khamis Hassan, Jaji Khamis Ramadhan Abdalla na Jokha Khamis Makame. 

 

Hafla ya kuapishwa kwa watendaji hao wa ZEC imefanyika leo Ikulu visiwani Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali, akiwemo Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd, Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar Kabih, na Kadhi Mkuu wa Zanzibar,  Sheikh Khamis Haji.

 

Wakizungumza baada ya kuapishwa, Himid ameahidi kutumia uzoefu wake katika masuala ya uchaguzi kuhakikisha anaiongoza tume hiyo kufuata Katiba, sheria na kanuni zilizopo bila kupendelea.