Dogo Janja: Sina mtoto wa nje ya ndoa

Mkali wa Bongo Fleva, Abdulaziz Abubakar ‘Dogo Janja’

Muktasari:

Amesema mpaka sasa ana uhakika hawezi kuletewa mtoto nje ya ndoa yake

Mkali wa Bongo Fleva, Abdulaziz Abubakar ‘Dogo Janja’ amesema mpaka sasa ana uhakika hawezi kuletewa mtoto nje ya ndoa yake kwa kuwa alikuwa mwangalifu katika uhusiano wa kimapenzi.

Akihojiwa katika kipindi cha Kikaangoni, Dogo Janja ambaye ni mume wa mcheza filamu, Irene Uwoya, alisema katika uhusiano wake alikuwa akitumia kinga, hivyo anaamini hakuna atakayemletea mtoto.

Kingine kilichomsaidia kuwa makini alisema imetokana na wasia kutoka kwa baba yake aliyemtaka asithubutu kupata mtoto kabla ya kuoa.

“Yaani mimi katika kitu nilikuwa makini ni kutembea na kinga kila nilipokwenda, hivyo hakuna mtu yoyote atakuja aniambie eti nina mtoto na yeye labda mke wangu Irene ninayeishi naye kwa sasa,” alisema.