EU kusaidia sekta ya viwanda

Muktasari:

Balozi wa EU nchini, Roealand Van der Greer alieleza azma hiyo jana akiongoza ujumbe wa mabalozi wa nchi za Ulaya kwenye ziara ya siku moja kukagua bandari hiyo.

Tanga. Umoja wa Ulaya (EU), umesema utaisaidia Bandari ya Tanga ili kuinua sekta ya viwanda na kukuza uchumi.

Balozi wa EU nchini, Roealand Van der Greer alieleza azma hiyo jana akiongoza ujumbe wa mabalozi wa nchi za Ulaya kwenye ziara ya siku moja kukagua bandari hiyo.

Alisema ziara hiyo ililenga kuangalia uwezekano wa kukuza sekta ya viwanda mkoani Tanga na kuboresha bandari hiyo.