EU yawakumbuka walimu

Muktasari:

  • Mwakilishi mkazi wa umoja huo, Olivier Coupleux alitoa taarifa hiyo jana wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili inayofanyika jijini hapa.

Dar es Salaam. Katika kuthamini na kuendeleza michango ya wabunifu nchini, Umoja wa Ulaya (EU) umetoa Sh145 milioni kwa ajili ya mafunzo ya walimu wa vyuo vikuu na taasisi kuandaa mitalaa itakayotumika kufundisha somo la haki miliki bunifu.

Mwakilishi mkazi wa umoja huo, Olivier Coupleux alitoa taarifa hiyo jana wakati wa ufunguzi wa semina ya siku mbili inayofanyika jijini hapa.

Alisema wabunifu wamekuwa chachu ya maendeleo katika nyanja mbalimbali.

“Tunaunga mkono jitihada za Rais John Magufuli katika kutambua mchango wa viwanda, wabunifu watakaojitokeza watafaidika na mpango huu utakaowafanya kujua haki zao na kunufaika kiuchumi,” alisema Coupleux.