Saturday, April 15, 2017

Ehud Barak atua nchini akisifia vivutio vilivyopo

Pichani Waziri mkuu mstaafu wa Esrael Ehud

Pichani Waziri mkuu mstaafu wa Esrael Ehud Barak akipokewa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii,Ramo Makani na Meneja uhusiano  wa TANAPA Pascal Shelutete katika eneo la Olduvai Ngorongoro ambapo yeye na familia yake Wapo nchini Kutalii. Picha Mussa Juma 

By Mussa Juma, Mwananchi ; Mjuma@mwananchi.co.tz

Ngorongoro. Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete amesema Waziri Mkuu mstaafu wa Israel, Ehud Barak amekuja nchini kutokana na kuvutiwa na vivutio vya utalii vilivyopo nchini, ikiwamo Hifadhi ya Serengeti yenye idadi kubwa ya nyumbu wahamao.

Akizungumzia ziara hiyo, Shelutete amesema ziara ya kiongozi aliyekuja na familia yake pamoja na watalii wengine zaidi 100, imefungua milango kwa Waisraeli kuitembelea Tanzania.

Amesema ujio za msafara wa kiongozi huyo unaonyesha kwamba Tanzania imejaliwa kuwa na vivutio vingi vinavyohitaji kutembelewa na wananchi pamoja wageni.

Naye Meneja Utalii wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro, Paul Fisoo alisema ziara ya Barak inathibitisha utajiri wa vivutio vya utalii vilivyopo nchini.

Awali, waziri mkuu huyo mstaafu alisema Tanzania imejaliwa kuwa na utajiri wa vivutio vya utalii ambavyo havipo katika nchi yoyote duniania.

-->