Elimu ya mpigakura kutolewa shuleni

Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima 

Muktasari:

Akizungumza wakati wa maonyesho ya 32 ya kitaifa ya Jumuiya ya Serikali za Mitaa (Alat) mjini Musoma, Mkurugenzi wa NEC, Kailima Ramadhani amesema tume pia imejipanga kuendelea kuitoa elimu hiyo kwenye mikutano ya Serikali na watu binafsi.

Musoma. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema itaanza kutoa elimu ya mpigakura nchini, ikiwamo kwenye shule zote za sekondari ikihusisha taasisi na asasi mbalimbali.

Akizungumza wakati wa maonyesho ya 32 ya kitaifa ya Jumuiya ya Serikali za Mitaa (Alat) mjini Musoma, Mkurugenzi wa NEC, Kailima Ramadhani amesema tume pia imejipanga kuendelea kuitoa elimu hiyo kwenye mikutano ya Serikali na watu binafsi.

Ramadhani amesema wanalenga kuongeza uelewa wa umuhimu wa upigaji kura ili kuondoa manung’uniko kutoka kwa wadau na vyama vya siasa.