VIDEO: Familia ya 'Mo Dewji': Tunamshukuru Rais Magufuli

Muktasari:

Familia ya bilionea Mohamed Dewji 'Mo' imewashukuru wote waliofanikisha kupatikana kwa kijana wao, husasan Rais John Magufuli

Msemaji wa familia, Azzim Dewji Azzim amesema, afya ya Mo ni nzuri asilimia 100


Dar es Salaam. Familia ya mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania, Mohamed Dewji 'Mo' imemshukuru Rais John Magufuli jinsi alivyofanikisha kupatikana kwa bilionea huyo kijana Afrika.

Msemaji wa familia, Azzim Dewji akizungumza nyumbani kwa 'Mo' leo asubuhi Jumamosi Oktoba 20, 2018 amesema,"Tumempata na tunamshukuru Mungu."

Amesema afya ya 'Mo' aliyetekwa alfajiri ya Alhamisi wiki iliyopita Oktoba 11,2018 jijini Dar es Salaam, Tanzania 'ni nzuri asilimia 100' sema labda sababu alitekwa inaweza kuwa tatizo kisaikolojia.

Azzim amesema,"Amepatikana mida ya saa 8.30 usiku, walimuacha halafu yeye (Mo) akapiga simu kwa baba yake."

"Tunamshukuru sana Rais (John Magufuli) kwa kuagiza vyombo vyake vya usalama na vyombo vyake tumempata," amesema Azzim

Msemaji huyo amesema baadaye kutakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaomhusisha 'Mo' Dewji.

Endelea kufuatilia MwananchiBilionea 'Mo' Dewji apatikana

Endelea kufuatilia Mwananchi