Familia yakubali kumzika ndugu yao aliyeuawa na polisi

Mkuu wa Mkoa wa Mara,  Adam Malima 

Muktasari:

Familia ya Edward Mahende (73) aliyeuawa kwa kupigwa risasi na Polisi wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamekubali kuchukua mwili wa ndugu yao kwa ajili ya maziko 

Serengeti. Familia ya Edward Mahende (73) aliyeuawa kwa kupigwa risasi na Polisi wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamekubali kuchukua mwili wa ndugu yao kwa ajili ya maziko.

Wamechukua uamuzi huo leo Jumanne Oktoba 16,2018 baada ya kufanya mazungumzo na mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu ikiwa zimepita siku nne tangu Mahende kuuawa.

Mahende alipigwa risasi na polisi Oktoba 12, 2018 nyumbani kwake baada ya kutoa mkuki kwa lengo la kumchoma inspekta wa polisi aliyekuwa akipiga hodi katika nyumba hiyo.

Alishambuliwa na askari polisi waliokuwa pamoja na isnpekta huyo.

Baada ya tukio hilo ndugu walisusa kuchukua mwili wakishinikiza kupewa maelezo ya kina juu ya kifo hicho.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumanne Oktoba 16, 2018  msemaji wa familia, Samson Gimase amesema wamekubali kuchukua mwili wa ndugu yao   baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari.

"Tukimaliza uchunguzi tutachukua mwili kwa ajili ya mazishi. Tumekubaliana na mkuu wa wilaya tuchukue taarifa ya daktari ambayo itatusaidia kufungua kesi dhidi ya jeshi la polisi maana wamekiri kumuua," amesema.

Amesema katika mawasiliano na Mkuu wa Mkoa wa Mara,  Adam Malima waliyoyafanya jana aliwataka kukutana na Babu kutafuta  muafaka kwa ajili ya mazishi.

Soma zaidi: