Thursday, March 16, 2017

Finland yasaini mkataba wa Sh3.9 bilioni na kampuni za misitu

Balozi wa Finland hapa nchini, Pekka Hukka  na

Balozi wa Finland hapa nchini, Pekka Hukka  na Mkurugenzi wa Kampuni ya misitu ya New Forest Company ,Agripina Mandiwona wakikabidhiana mkataba wa mradi wa upandaji miti. 

By Cledo Michael, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ubalozi wa Finland nchini umesaini mkataba wa makubaliano wa jumla ya Euro 1.6 milioni (bilioni 3.9) na kampuni mbili za  misitu, ili kuwawezesha wakulima kupanda miti kwa ajili ya biashara.

Kampuni hizo ni New Forest Company(NFC) na Kilombelo Valley Teak Company(KVTC) ambapo  makubaliano hayo ni ya miaka mitatu ya uendeshaji wa mradi huo utakaowezesha kupanda hekta 2000 za miti katika Maeneo ya Iringa,Njombe,Mbeya na Morogoro.

Akizungumza leo(Alhamisi) Balozi wa Finland hapa nchini, Pekka Hukka amesema kiasi hicho cha fedha kitawezesha kuongeza kasi ya upandaji miti kwa wakulima wadogo wakati kampuni hizo zikiwa mteja wa miti hiyo.

"Asilimia 50 imetolewa na Serikali(Finland) na Makampuni yametoa asilimia 50.Mradi huu utasaidia kutunza maliasili pamoja na kukuza kipato cha wakulima wadogo,"amesema balozi huyo.

-->