Foleni Dar yaichanganya Serikali

Muktasari:

Mpango huo ulijikitika kwenye kuboresha na kujenga barabara, zikiwamo za magari ya mwendo kasi, za juu na Daraja la Mwalimu Nyerere eneo la Kigamboni.

Dar es Salaam. Serikali imerudia kufanya tathimni ya mpango mkakati wa mwaka 2008 uliodhamiria kujenga miundombinu ili kuboresha usafiri na kupunguza foleni ya magari jijini Dar es Salaam.
Mpango huo ulijikitika kwenye kuboresha na kujenga barabara, zikiwamo za magari ya mwendo kasi, za juu na Daraja la Mwalimu Nyerere eneo la Kigamboni.
Licha ya baadhi ya barabara na Daraja la Mwalimu Nyerere kukamilika na ujenzi wa barabara ya juu eneo la Tazara ukiendelea, bado inaonekana tatizo la foleni Dar es Salaam halijapungua.
Hata hivyo, imeelezwa kuwa hali hiyo inachangiwa na kasi ya ongezeko la watu  na magari jijini hapa. Akizungumza jana katika kikao kilichowakutanisha wadau mbalimbali likiwamo Shirika la Maendeleo la Japan (Jica),