#WC2018: Fuatilia fainali za Kombe la Dunia ukiyajua haya

Muktasari:

Takwimu na matukio haya yanasaidia kuelewa mambo yatakayokuwa yakitokea uwanjani yanamaanisha nini katika rekodi za historia ya Kombe la Dunia.


Rekodi na Takwimu

5.4 – Kiwango cha juu cha wastani wa kufunga mabao kwa mechi moja kilikuwa mwaka 1954 wakati Uswisi ilipokuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia.

68,991 - Wastani wa idadi ya watu walioingia uwanjani kuangalia mechi za Kombe la Dunia ulikuwa mwaka 1994 wakati zilipofanyika Marekani.

171 – Ufaransa mwaka 1998 na Brazil (2014) zote zilifikia kiwango hicho cha juu cha kufunga mabao katika awamu moja ya michuano ya Kombe la Dunia (kuanzia mechi ya kufuzu).

5 na 70 na 20 – Brazil imetwaa Kombe la Dunia mara nyingi zaidi kuliko nchi nyingine, Imetwaa mara tano(1958, 1962, 1970, 1994, na 2002). Pia, Brazil inaongoza kwa kushinda mechi nyingi (70) na inaongoza kwa kushiriki fainali za Kombe la Dunia mara nyingi (20). Fainali za Russia ni mara ya 21.

8 na 4 na 106 – Ujerumani (ikijumuishwa na Ujemarumani Magharibi) imeshiriki mara nane lakini imefika fainali mara nne, ambayo pia ni rekodi. Ujerumani pia imecheza mechi nyingi zaidi kwenye fainali za Kombe la Dunia kuliko taifa jingine (106).

25 - Hakuna timu iliyoonja machungu ya vipigo vingi kwenye fainali za Kombe la Dunia kama Mexico. Imefungwa mara 25.

4 – Nchi nne zimecheza fainali za Kombe la Dunia lakini zimepoteza mechi zote na kushindwa kuziona nyavu– Canada, China PR, Indonesia na Congo DR.

9 – Idadi kubwa ya mechi ambayo Honduras ilicheza bila ya kushinda.

224 na 121 – Ujerumani, kwa mara nyingine na safari hii ni idadi kubwa ya magoli iliyofunga (224) na kuruhusu (121) kwenye michuano ya Kombe la Dunia.

21 – Italia ndiyo nchi inayoongoza kwa kutoka sare mechi nyingi (21).

10 – Wachezaji 10 wa Brazil wameonyeshwa kadi nyekundu kwenye fainali za Kombe la Dunia.

111 – Argentina inaongoza kwa wachezaji wake kuonyeshwa kadi za njano (111).

5 – Argentina imefikia hatua ya kuamua mshindi kwa penati mara nyingi zaidi (mara tano) kwenye Kombe la Dunia kuliko nchi nyingine. Katika kupigiana penati imepoteza mchezo mmoja.

3 – England na Italia ndiyo zinaongoza kwa kupoteza michezo yao kwa njia ya penati tano.

5 – Rekodi ya kushiriki mara nyingi fainali za Kombe la Dunia inashikiliwa kwa pamoja na kipa wa Mexico, Antonio Carbajal na kiungo wa Ujerumani, Lothar Matthaeus.  Beki wa Mexico, Rafael Márquez atafikia rekodi hiyo katika fainali za mwaka huu kama akichezeshwa. Gianluigi Buffon angefikia rekodi hiyo kama angecheza kwenye fainali za Kombe la Dunia za Ufaransa mwaka 1998.

25 – Hakuna mchezaji aliyecheza mechi nyingi za fainali za Kombe la Dunia zaidi ya Lothar Matthaeus, aliyecheza mechi 25.

17 na 16 na 14 – Miroslav Klose alicheza fainali za mwaka 2002, 2006, 2010, na 2014 na hakuna mchezaji amemaliza mechi nyingi (17) akiwa kwenye timu iliyoshinda zaidi yake. Klose pia anaongoza kwa kufunga mabao mengi kwenye fainali za Kombe la Dunia. Alifunga mabao 16 nchini Brazil. Pia amecheza mechi nyingi za mtoano (14) katika fainali kuliko mchezaji mwingine.

Miaka 43, mwezi 0 na siku tatu – Kipa wa Colombia, Faryd Mondragon ni mchezaji aliyeshiriki fainali za Kombe la Dunia akiwa na umri mkubwa, miaka 43. Alicheza wakati Colombia ilipoifunga Japan mabao 4-1 katika fainali za mwaka 2014 nchini Brazil. Kipa wa Misri, Essam El-Hadary anaweza kuvunja rekodi hiyo iwapo atachezeshwa fainali za Russia wakati Misri itakapoivaa Uruguay. Ana umri wa miaka 45.  El-Hadary pia ataweza rekodi ya kucheza kwa mara ya kwanza fainali hizo akiwa na umri mkubwa.

 Miaka 17, mwezi mmoja na siku kumi – Norman Whiteside wa Manchester United aliichezea Ireland ya Kaskazini katika mechi dhidi ya Yugoslavia na anaendelea kuwa mchezaji mwenye umri mdogo kuliko wote kucheza fainali za Kombe la Dunia.

 5 – Kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Marekani mwaka 1994, Oleg Salenko alifunga mabao matano wakati Russia ilipoizamisha Cameroon kwa mabaop 6-1. hakuna mchezaji anayemzidi kwa kufunga mabao mengi katika mechi moja ya fainali za Kombe la Dunia.

 4 – Mshambuliaji wa Poland, Ernest Wilimowski alicheza mechi moja tu ya fainali za Kombe la Dunia lakini aliweka rekodi mbili. Hakuna mchezaji anayeweza kufikia wastani wa mabao kwa mechi. Licha ya kufunga mabao manne (pia alifanyiwa faulo iliyosababisha penati iliyozaa bao baada ya mchezaji mwenzake kuipiga), alimaliza mchezo huo huku timu yake ikilala kwa mabao 6-5 mbele ya Brazil nchini Ufaransa mwaka 1938 baada ya timu hizo kuongezewa muda.

6 - Idadi kubwa ya kadi walizoonyeshwa wachezaji kwenye fainali za Kombe la Dunia– Zidane (Ufaransa), Cafu (Brazil), na Rafael Marquez (Mexico). Kwa wastani Zidane ameonyeshwa kadi mara sita katika mechi 12 tu.

2 - Zidane na beki wa Cameroon, Rigobert Song walionyeshwa kadi nyekundu mara mbili katika fainali za Kombe la Dunia.

3 - Ni Pele pekee aliyetwaa Kombe la Dunia mara tatu - 1958, 1962, 1970.

2,217 – Idadi ya dakika ambazo Paolo Maldini amechezakatika mechi za Kombe la Dunia.

16 na 1 – Diego Maradona ameiongoza nchi yake akiwa nahodha mara nyingi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia.