Gambo amwita DC kikaangoni

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo

Muktasari:

Chalya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, ni miongoni mwa wakurugenzi 22 walioteuliwa na Rais John Magufuli Juni 26 kuwa wakuu wa wilaya.

Longido. Baada ya mradi wa maji kujengwa chini ya kiwango wilayani hapa, Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ameagiza aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Longido, Julius Chalya kurudi katika kituo hicho kutoa ufafanuzi.

Chalya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, ni miongoni mwa wakurugenzi 22 walioteuliwa na Rais John Magufuli Juni 26 kuwa wakuu wa wilaya.

Hata hivyo, Chalya alikiri mradi huo kujengwa chini ya kiwango na kulazimika kuunda kamati mwaka 2014 iliyotoa taarifa ya maandishi kwa halmashauri.

Alisema taarifa hiyo ina majibu yote yanayoweza kutumika kuona sababu za kukwama na watu wanaotakiwa kuchukuliwa hatua. Alisema kabla ya kuondoka alikabidhi taarifa yote kwa mkurugenzi mtendaji mpya.