VIDEO: Gari lililotumika kumteka Mo Dewji lapelekwa kituo cha polisi

Muktasari:

Gari aina ya Toyota Surf iliyotumika kumteka mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ limepelekwa kituo cha polisi cha Oysterbay


Dar es salaam. Gari aina ya Toyota Surf iliyotumika kumteka mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ limepelekwa kituo cha polisi cha Oysterbay.

Gari hilo lilitelekezwa leo Oktoba 20, 2018 saa nane usiku baada ya watekaji hao kumuachia mfanyabiashara huyo katika viwanja vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amesema watekaji hao walijaribu kulichoma moto gari hilo lilikuwa na bunduki ya kivita aina ya AK 47 na bastola tatu, bila mafanikio.

Uchunguzi wa awali wa polisi umeonyesha gari hilo lenye namba za usajili za nje ya Tanzania, liliingia nchini Septemba mosi, 2018.

Mo Dewji alitekwa alfajiri ya Oktoba 11, 2018 katika Hoteli ya Colosseum alikokwenda kwa ajili ya kufanya mazoezi na tangu wakati huo hakukuwa na taarifa zozote za wapi alipo hadi leo alipotelekezwa katika viwanja hivyo na kuwasiliana na baba yake, Gullam Hussein baada ya kupata msaada wa simu.