Gereza laomba wafungwa zaidi

Muktasari:

Miongoni mwa pembejeo hizo ni majembe, matrekta na mitambo mingine ya kilimo.

Mbeya. Mkuu wa Gereza la Kilimo Songwe,  Lyzeck Mwaseba ameiomba Serikali kulipatia wafungwa wengi na pembejeo ili kuongeza uzalishaji.
Miongoni mwa pembejeo hizo ni majembe, matrekta na mitambo mingine ya kilimo.
Mwaseba  aliwasilisha ombi hilo mbele ya Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliyotembelea gereza hilo ikiambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni.Ziara hiyo ililenga kujionea uzalishaji wa mahindi unaofanya na wafungwa.
“Gereza hili lina ukubwa wa hekta 2,170, lakini hivi sasa zinalimwa eka 250 kutokana na kuwapo wafungwa 165 tu ambao ni wachache,’’ alisema.