Tambwe kuzikwa Dar

Muktasari:

Amesema kwa sasa yeye na wana Chadema wapo msibani nyumbani kwa Tambwe Mbagala Kizuiani.


Dar es Salaam. Kada wa Chadema, Richard Tambwe Hiza aliyefariki dunia leo asubuhi Februari 8, 2018 anatarajiwa kuzikwa Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili leo, Katibu wa Chadema wa Dar es Salaam Kuu, Henry Kileo amesema: “Tambwe atazikwa hapa Dar es Salaam, ni lini na wapi tutawajulisha.”

Kuhusu kufanyika kwa kampeni au la za ubunge wa Kinondoni, Kileo amesema suala hilo lipo chini ya Chadema Makao Makuu na kwamba viongozi wake wapo kwenye kikao kujadili hilo na watakuja na majibu.

Amesema kwa sasa yeye na wana Chadema wapo msibani nyumbani kwa Tambwe Mbagala Kizuiani.