Griezmann atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka

Muktasari:

Nyota huyo mwenye miaka  25 alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo mjini Valencia juzi, lakini alishindwa kuhudhuria hafla ya kupokea tuzo hiyo.

Madrid, Hispania. Mshambuliaji wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann, raia wa Ufaransa ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Ligi Kuu ya Hispania, La Liga msimu uliopita.

Nyota huyo mwenye miaka  25 alitangazwa mshindi wa tuzo hiyo mjini Valencia juzi, lakini alishindwa kuhudhuria hafla ya kupokea tuzo hiyo.

Klabu ya Atletico pia ilikuwa yenye furaha kubwa baada ya kuzoa tuzo zaidi kupitia kocha wake,  Diego Simeone aliyeteuliwa kocha bora wa mwaka, kipa Jan Oblak na beki Diego Godin  walioshinda tuzo za ulinzi imara.