Gwajima atoa neno kanisani

Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Uzima na Ufufuo.

Muktasari:

  • Askofu huyo aliyeondoka nchini Juni 15 kwenda Japan, alikuwa akitafutwa na Jeshi la Polisi baada ya kusambaa kwa sauti iliyorekodiwa ikihusishwa naye, ikitoa tuhuma za kuwapo mipango ya kumzuia Rais John Magufuli asipewe uenyekiti wa CCM kutokana na kazi anayoifanya ya kushughulikia mafisadi.

Dar es Salaam. Askofu Josephat Gwajima wa Kanisa la Uzima na Ufufuo ameshiriki misa pamoja na waumini wake.

Askofu huyo aliyeondoka nchini Juni 15 kwenda Japan, alikuwa akitafutwa na Jeshi la Polisi baada ya kusambaa kwa sauti iliyorekodiwa ikihusishwa naye, ikitoa tuhuma za kuwapo mipango ya kumzuia Rais John Magufuli asipewe uenyekiti wa CCM kutokana na kazi anayoifanya ya kushughulikia mafisadi.

Kwenye misa hiyo ya kwanza tangu arejee nchini, Gwajima hakuizungumzia Serikali wala taasisi zake na badala yake alijikita kutoa mafundisho ya kuwajenga waumini wake kuweza kukabiliana na changamoto za duniani zinazokwamisha maendeleo yao kiroho na kimwili.

"Mwenyezi Mungu habadili mipango yake. Ni binadamu pekee ndiye anaweza kukupa leo na akakunyang’anya kesho,” amesema wakati akihubiri.