Hatimaye Jecha afunguka

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Salim Jeecha

Muktasari:

Akihojiwa katika kipindi cha Funguka cha Azam TV jana, Jecha alisema hakutoa taarifa ya awali kwa Dk Shein kuhusu kufuta matokeo hayo na wala hana namba yake ya simu.

Dar es Salaam. Baada ya kimya cha muda mrefu, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jeccha Salim Jeecha amesema hakumshirikisha Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2015 visiwani humo.

Akihojiwa katika kipindi cha Funguka cha Azam TV jana, Jecha alisema hakutoa taarifa ya awali kwa Dk Shein kuhusu kufuta matokeo hayo na wala hana namba yake ya simu.

“Hata simu yake siifahamu, wala nambari (namba) yake ya simu siijui, mimi nilikuwa na timu yangu tu basi,” alisema Jecha.

Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar yalifutwa Oktoba 28, mwaka 2005, siku ambayo Jecha ilikuwa atangaze matokeo ya mshindi wa urais na majimbo yaliyokuwa yamebakia.