Hatukuikashifu Serikali- Bavicha

Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa.

Muktasari:

  • Vijana hao ni Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa; Katibu Mkuu, Julius Mwita na Mwenyekiti wa baraza hilo Mkoa wa Mbeya, George Tito wanaokabiliwa na kesi ya kuikashifu Serikali. Wanatetewa na mawakili Isaac Mwaipopo na John Chigongo.

Dodoma. Viongozi wa Baraza la Vijana Chadema (Bavicha) wamesema hawakuvaa fulana ili kuikashifu Serikali bali kama nguo nyingine ya kawaida.

Vijana hao ni Patrobas Katambi, Mwenyekiti wa Bavicha Taifa; Katibu Mkuu, Julius Mwita na Mwenyekiti wa baraza hilo Mkoa wa Mbeya, George Tito wanaokabiliwa na kesi ya kuikashifu Serikali. Wanatetewa na mawakili Isaac Mwaipopo na John Chigongo.

Mwita akijitetea juzi, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Dodoma, James Karayemaha amedai Julai 8, pamoja na wenzake walikwenda Dodoma wakitoka Musoma na usiku walikuwa kwenye baa ya Cape Town kwa ajili ya kupata chakula.

Wakiwa hapo alidai polisi walifika na kuwataka kwenda kituoni walikopigwa picha na kuwekwa rumande.