Hillary Clinton aandika historia mpya Marekani

Hilary Clinton amekuwa mwanamke wa kwanza kuandika historia nchini Marekani baada ya usiku huu kupitishwa rasmi na chama chake cha Democratic kuwania nafasi ya Urais.

Muktasari:

  • Mpinzani wake kwenye kinyang’anyiro hicho kupitia chama cha Democratic alikuwa Bernie Sanders.

Marekani. Hilary Clinton amekuwa mwanamke wa kwanza kuandika historia nchini Marekani baada ya usiku huu kupitishwa rasmi na chama chake cha Democratic kuwania nafasi ya Urais.

 Mpinzani wake kwenye kinyang’anyiro hicho kupitia chama cha Democratic alikuwa Bernie Sanders.

Hilary ambaye ni mke wa Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, sasa anaanza rasmi safari ya kwenda kupambana na mpinzani wake wa chama cha Republican, Donald Trump.

Hata hivyo, Mpinzani wake mkuu ndani ya Democratic, Bernie Sanders alimaliza mchakato wa kuwania nafasi hiyo kwa kuwataka wajumbe kumchagua Hilary kwa kauli moja.