Hood yapiga hodi baa

Muktasari:

Gari hilo liliacha njia saa 9: 00 usiku likiwa linavutwa kwenda gereji, lakini likamshinda dereva kwenye kona

Arusha. Basi la Hood linalofanya safari za Arusha - Mbeya lililokuwa linavutwa na gari aina ya Fuso limeacha njia na kuingia kwenye baa ya Ngarenaro Top Inn.

Gari hilo liliacha njia saa 9: 00 usiku likiwa linavutwa kwenda gereji, lakini likamshinda dereva kwenye kona

Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Hood, Masange Kilua amesema hakuna maafa yaliyotokea zaidi ya dereva wa gari hilo kupata jeraha mguuni na uharibifu kwenye baa hiyo.