Idadi ya wanufaika mikopo ya elimu ya juu yafikia 113,478

Muktasari:

Wanafunzi 20,183 wamepangiwa mikopo baada ya kukamilika kwa uchambuzi wa maombi ya mikopo 88,163 yaliyopokewa hadi kufikia Agosti 11, na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB).

Dar es Salaam. Idadi ya wanafunzi watakaonufaika na mikopo kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 imefikia 113,478 kutoka 93,295, baada ya wanufaika 20,183 wapya kuingizwa katika utaratibu huo. 

Wanafunzi 20,183 wamepangiwa mikopo baada ya kukamilika kwa uchambuzi wa maombi ya mikopo 88,163 yaliyopokewa hadi kufikia Agosti 11, na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB).

Akifafanua kuhusu wanafunzi hao wapya waliodahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Mkurugenzi Mtendaji wa HELSB, Abdularazaq Badru alisema jana kuwa kati ya wanafunzi 58,010 waliodahiliwa na kwa majumuisho ya majina yaliyokuwa yanatoka kwa makundi, waombaji wapya 20,183 wamepangiwa kupata mikopo.