Saturday, January 13, 2018

Kampuni ya PwC yafungiwa India

Kampala, Uganda. Kampuni ya Kimataifa ya Uhasibu ya PricewaterhouseCoopers (PwC), moja ya makampuni maarufu duniani imefungiwa miaka miwili kufanya ukaguzi wa hesabu nchini India baada ya kushindwa kubaini ufisadi wa Dola za Marekani 1.7 katika shirika la huduma za kompyuta la Satyam.

Kibano hicho cha India, kimesababisha wasiwasi nchini Uganda ambako PwC ni moja ya mashirika yaliyofanya ukaguzi wa vitabu vya akaunti za Benki ya Crane kabla ya kuwekwa chini ya uangalizi wa Benki Kuu (BoU).

Gazeti la Daily Monitor limefahamishwa kwamba wakati Fulani Benki ya Crane Bank iliwahi kukaguliwa na KPMG, PwC na Deloitte and Touch.

Ukaguzi kufanywa na makampuni ya nje ni matakwa ya kisheria chini ya kifungu 4 (2) cha Taasisi za Fedha ya mwaka 2010. Ripoti iliyotolewa na ya PwC Januari 13, 2017 kuhusu Benki ya Crane imesababisha kesi mahakamani ambako BoU na Ruparelia wanashtakiana.

 

-->