JB: Tulichelewa kumtumia Mzee Majuto

Waombolezaji wakiwa wamebeba mwili wa mwigizaji nguli wa vichekesho nchini, Mzee King Majuto baada ya swala ya kumuombea iliyofanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam leo. Picha na Ericky Boniphace

Muktasari:

Mzee Majuto alifariki dunia jana Agosti 9 saa 2 usiku Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.


Dar es Salaam. Msanii wa filamu Jacob Steven (JB) amesema wasanii walichelewa kumtumia mzee Majuto kutokana na kipaji alichojaliwa

Akizungumza leo Agosti 9 wakati kuuaga mwili wa Mzee Majuto katika viwanja vya Karimjee, JB amesema pamoja na kuwahi kucheza naye filamu mbili, ikiwamo; ‘Shikamoo Mzee’ na  ‘Nakwenda kwa mwanangu’, lakini anaona bado wasanii hawakumtumia ipasavyo.

Amesema licha ya Mzee Majuto Mzee  kuigiza kwa miaka mingi lakini bado  hakuchosha machoni mwa watu na ndiyo maana filamu zake zote zilifanya vizuri.

JB amesema kifo cha Majuto kimemfunza mengi ikiwamo kuipenda sanaa kama kazi kwani ndizo zilizomfanya akapata mafaniko mbalimbali ikiwamo ya kufanya matangazo.

"Mzee Majuto ametufundisha kwamba tukiiheshimu kazi ya filamu tunaweza kuwa na mafanikio mengi kuliko tunavyofikiria na kubaki kulalamika kila siku, kwani vitu vingi alivyokuwa akivimiliki vya maendeleo vimetokana na Sanaa hii," amesema JB.

Soma Zaidi: