JKCI yalalamikia ufinyu wa eneo

Muktasari:

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya taasisi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema kwa mwaka 2016 pekee Sh150 milioni zimetumika mwaka Jana kwa ajili ya kuwalipia wagonjwa wa msamaha.

Dar es Salaam.Uwezo Mdogo wa wagonjwa kulipia gharama za matibabu ya magonjwa ya moyo na ufinyu wa eneo vimekuwa ni changamoto kubwa kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya ya Kikwete (JKCI).

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya taasisi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema kwa mwaka 2016 pekee Sh150 milioni zimetumika mwaka Jana kwa ajili ya kuwalipia wagonjwa wa msamaha.

Alisema JKCI imekuwa ikipokea idadi kubwa ya wagonjwa kwa kadri miaka inavyosonga, hivyo kushauri fedha zilizokuwa zikipeleka wagonjwa nje ya nchi, zielekezwe katika kuitanua taasisi hiyo ili kutoa huduma kwa Watanzania wengi zaidi.