JNIA yadaiwa uchochoro wa nyara

Muktasari:

Kamanda wa Polisi wa JNIA, Martine Otieno  alisema pia, madini na dawa za  kulevya hukamatwa uwanjani hapo.

Dar es Salaam. Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), umetajwa kuwa miongoni mwa maeneo yanayotumiwa zaidi kupitisha nyara za Serikali kwa njia za magendo, zikiwamo bidhaa zinazotengenezwa kwa  meno ya tembo.

Kamanda wa Polisi wa JNIA, Martine Otieno  alisema pia, madini na dawa za  kulevya hukamatwa uwanjani hapo.

Otieno alisema Januari hadi Desemba mwaka jana yalikuwapo matukio 20 ya kukamatwa kwa nyara za Serikali ambazo zilikuwa zikisafirishwa pasipo kuwa na vibali, huku mwaka 2015 yaliripotiwa matukio 29.

Akizungumzia dawa za kulevya, alisema yalikuwapo matukio sita ya watu waliojaribu kupitisha mihadarati hiyo uwanjani hapo mwaka jana.