JPM agoma kuanzisha mikoa, wilaya mpya

Rais John Magufuli.

Muktasari:

Akizungumza na wakazi wa mji wa Nzega ambako wabunge hao walitoa ombi hilo, Magufuli alisema hana mpango wa kugawa mkoa wala wilaya kwa kuwa kufanya hivyo ni kuongeza gharama za uendeshaji wa shughuli za Serikali.

Igunga. Rais John Magufuli amewagomea baadhi ya wabunge waliopendekeza Tabora kugawanywa kwa kuanzisha mkoa mpya wa Nzega.

Wabunge hao ni Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamisi Kigwangalla ambaye pia ni mbunge wa Nzega Vijijini, Hussein Bashe (Nzega Mjini) na  Seif Gulamali wa Manonga.

Akizungumza na wakazi wa mji wa Nzega ambako wabunge hao walitoa ombi hilo, Magufuli alisema hana mpango wa kugawa mkoa wala wilaya kwa kuwa kufanya hivyo ni kuongeza gharama za uendeshaji wa shughuli za Serikali.

Badala yake alisema fedha ambazo zingetumika kuanzisha mikoa na wilaya mpya zitaelekezwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Zaidi soma Gazetu letu la Mwananchi