JPM amteua Dk Mduma mwenyekiti wa CMSA

Rais John Magufuli

Muktasari:

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dk   Mduma umeanza  Februari 23, mwaka huu.

Dar es Salaam. Rais John  Magufuli leo (Ijumaa) amemteua Dk  John Mduma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA).

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dk   Mduma umeanza  Februari 23, mwaka huu.

Dk Mduma anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Grace Rubambey ambaye amemaliza muda wake.