JPM ashauriwa kukutana na viongozi wa kisiasa

Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Benson Bana.

Muktasari:

Kauli ya Profesa Bana imetolewa wakati vyama vya siasa vikimshutumu Rais Magufuli kwa kuvibana baada ya Serikali yake kupiga marufuku mikutano yote ya vyama na badala yake akisema siasa za majukwaani zifanyike 2020 wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Dar es Salaam. Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Benson Bana amesema endapo angepata fursa ya kuonana na Rais John Magufuli angemshauri aondoe ukuta uliopo baina yake na viongozi wengine wa kisiasa kwa kukaa meza moja ya mazungumzo hasa kwa mambo ya msingi ya nchi.

Kauli ya Profesa Bana imetolewa wakati vyama vya siasa vikimshutumu Rais Magufuli kwa kuvibana baada ya Serikali yake kupiga marufuku mikutano yote ya vyama na badala yake akisema siasa za majukwaani zifanyike 2020 wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Profesa Bana ambaye alikuwa akijibu swali la mwandishi wetu kuhusu jambo ambalo angemshauri Rais endapo angepata wasaa wa kukutana naye alisema: “Atengeneze jukwaa litakalokuwa linamwezesha kukutana na viongozi wenzake wa kisiasa, aitishe hata mkutano ili wajadili mambo muhimu. Anaweza kuongea na viongozi wenye vyama vyenye wabunge au vyama vyote vya kisiasa, hili ni suala muhimu sana.”