JPM ateta na Mkapa Ikulu

Rais John Magufuli (kushoto) na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin  Mkapa (kulia). Picha na Maktaba

Muktasari:

Rais Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kumpa taarifa juu ya kazi anayoendelea kuifanya ya kuwa mwezeshaji wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.

Dar es Salaam. Rais John Magufuli  amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin  Mkapa Ikulu jijini hapa, leo (Alhamisi).

Rais Mkapa amesema lengo la kukutana na Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kumpa taarifa juu ya kazi anayoendelea kuifanya ya kuwa mwezeshaji wa mazungumzo ya mgogoro wa kisiasa nchini Burundi.

Pia, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maendeleo wa Denmark, Martin Bille Herman, Ikulu jijini hapa na kujadili kuhusu uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Denmark.

Katika mazungumzo hayo yaliyohudhuriwa na Balozi wa Denmark nchini Einar Hebogard, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, wamekubaliana kuimarisha zaidi ushirikiano   katika masuala ya maendeleo ya kiuchumi.