Saturday, August 12, 2017

JPM ateua Mkurugenzi Mkuu NHIFMkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga 

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga  

By Mwandishi Wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua, Bernard Konga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Konga umeanza Agosti 9, 2017.

Kabla ya uteuzi huo Konga alikuwa akikaimu nafasi hiyo.

 

-->