JPM awahakikishia ajira wanafunzi wa Udom

Rais Magufuli 

Dodoma. Rais John Magufuli amewahakiishia ajira wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma, (Udom) kutokana na ajira zilizokuwa zikishikiliwa na watumishi wenye vyeti feki.

Rais amesema watumishi  waliobainika na vyeti vya kughushi wafukuzwe kazi mara moja na wasilipwe mishahara yao ya mwezi huu.