JPM awasili viwanja vya Jamhuri kwa sherehe za Muungano

Rais John Magufuli 

Muktasari:

Viongozi wengine, wakiwamo mawaziri na wabunge walifika katika uwanja huo kuanzia saa 1:20 hadi saa 1:30 asubuhi.

Dodoma. Rais John Magufuli amewasili katika viwanja vya Jamhuri kwa ajili maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Muungano.

Rais amewasili saa 3; 15 akiwa kwenye gari la wazi.

Viongozi wengine, wakiwamo mawaziri na wabunge walifika katika uwanja huo kuanzia saa 1:20 hadi saa 1:30 asubuhi.

Kiongozi wa kwanza kuwasili ni Waziri Kiongozi Mstaafu Shamsi Vuai Nahodha ambaye alifika saa 1:25 asubuhi akifuatiwa na Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela aliyefika saa 1:30 asubuhi.

Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete aliwasili saa 2:20 asubuhi.

Uwanja wa Jamuhuri umepambwa kwa rangi  za bendera  ya Taifa na watu wote wanaoingia wamegawiwa bendera  za Taifa ndogo za mkononi.

Watu walianza kuingia uwanjani saa 12: 30 asubuhi kwa kutumia mageti kadhaa ambayo yalipangwa kutumika  kwa ajili ya kupita wageni.