JPM awateua Kabudi, Bulembo kuwa wabunge

Alhaji Abdallah Bulembo akisalimiana na Rais John Magufuli.Picha ya Maktaba

Muktasari:

  • Rais John Pombe Magufuli, leo amewateua Profesa Palamagamba Kabudi na Alhaji Abdallah Bulembo  kuwa  wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dar es Salaam. Rais John Pombe Magufuli, leo amewateua Profesa Palamagamba Kabudi na Alhaji Abdallah Bulembo  kuwa  wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 Taarifa iliyoletwa na Kitengo cha Mawasiliano cha Ikulu leo, imeeleza kuwa wabunge hao wateule wataapishwa kwa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia, Rais Magufuli amemteua Benedicto Martin Mashiba kuwa Balozi.

Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Balozi Mteule Benedicto Martin Mashiba vitatangazwa baadaye.