JPM kila kona

Rais John Magufuli

Muktasari:

  • Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli alieleza mikakati yake ikiwamo kuimarisha chama, kuboresha masilahi ndani ya chama, kuhamishia Serikali Dodoma na kupambana na rushwa na wasaliti ndani ya chama.

Dar/Mikoani. Siku moja baada ya Mwenyekiti mpya wa CCM, Rais John Magufuli kutoa hotuba iliyobainisha mikakati yake ndani ya chama, baadhi ya wasomi wamekuwa na maoni tofauti huku baadhi ya wapinzani wakisema imewatisha.

Katika hotuba hiyo, Rais Magufuli alieleza mikakati yake ikiwamo kuimarisha chama, kuboresha masilahi ndani ya chama, kuhamishia Serikali Dodoma na kupambana na rushwa na wasaliti ndani ya chama.

Mshauri wa ACT-Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo alisema ilikuwa hotuba nzuri lakini yenye tatizo la uchaguzi wa maneno.

Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro ametahadharisha kuhusu kauli ya Rais Magufuli ya kuhamia Dodoma ndani ya miaka mitano ni ngumu kwa kuwa jambo hilo linahitaji maandalizi na fedha za kutosha.